Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, kutokana na mnasaba wa kuingia Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka 1447 Hijria, Jameh Modarresin Hawza Ilmiyya Qom, imetoa maelekezo kuwaelwkea wahubiri na wanafunzi wa elimu za Kiislamu.
Jameh Modarresin Hawza Ilmiyya Qom, imewataka wahubiri katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, kwa kuwalingania watu, viongozi na watu mashuhuri katika jamii, kushikamana na uchamungu (taqwa) na umoja, kuongeza uimara na mshikamano wa kitaifa pamoja na kuimarisha uhusiano kati ya wananchi na viongozi; na watumie kwa kiwango cha juu uwezo na nafasi ya misikiti katika kueneza utamaduni wa ihsani na utoaji (sadaka na misaada) na kuwahudumia wenye uhitaji.
Aidha, wahubiri wanatakiwa kuwafafanulia watu, hasa vijana balehe na vijana kwa ujumla, vipengele vya mapinduzi ya Kimarekani–Wazayuni pamoja na vita vya kiutambuzi na vita mseto; na kwa kubainisha sura halisi ya adui na kuongeza mwamko wa utambuzi sahihi, watoe fursa ya kurejea kwa wale waliopotoshwa au kudanganywa.


Maoni yako